Language

Marekani na Tanzania zimeshirikiana kwa miongo kadhaa kushughulikia mahitaji muhimu ya afya, kwa kuzingatia huduma bora zilizojumuishwa, uimarishaji wa mifumo ya afya, na mienendo ya afya bora. Jitihada hizi zinaunga mkono juhudi za Tanzania za kuboresha mchango wa afya na huduma za afya, ikizingatia ufanisi na uwajibikaji. Mchango wa USAID kwa Serikali ya Tanzania ni pamoja na kufadhili miradi ya kupambambana na VVU / UKIMWI, malaria, kifua kikuu, uzazi wa mpango, afya ya uzazi, lishe, usalama wa afya duniani, na afya ya mama, watoto, na afya ya watoto.