Language

Miradi ya USAID ya Afya ya  mama na mtoto (MCH)  nchini Tanzania inaendelea kusaidia jitihada za kuzuia na kutokea Vifo vya Mtoto na vile vitokanavyo na Uzazi, ikitoa  kipaumbele cha kuboresha afya ya wanawake walio katika mazingira magumu, wasichana, watoto wachanga, na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Katika ngazi ya kitaifa, USAID inatoa usaidizi wa kitaalam kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Tanzania bara na kuwezesha utoaji wa huduma za kuokoa maisha kwa akina mama, watoto wachanga, na watoto upande wa Zanzibar. Mifano ya usaidizi wa kitaalamu ni pamoja na kuandaa miongozo ya kliniki ya kujifungua kabla ya wakati, kutibu maambukizi kwa watoto wachanga.