Language

 

Tanzania ni moja ya nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi barani Afrika, ikiwa na takriban asilimia 7 ya ukuaji wa Pato la Taifa kila mwaka tangu mwaka 2000. ,Walakini kwa sehemu kubwa umasikini bado upo. Karibu nusu ya Watanzania wanaishi chini ya dola 1.90 kwa siku. Ukuaji mkubwa wa idadi ya watu na uzalishaji mdogo katika sekta zinazotumia nguvukazi kubwa kama kilimo, ambacho huajiri asilimia 75 ya idadi ya watu, hupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi. Pamoja na hayo wakati maliasili za Tanzania ni muhimu kwa nchi na husaidia ustawi wa maisha ya Watanzania wengi, matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali hizi yanatishia kuendeleza mzunguko wa umaskini.

Kwa kuunga mkono lengo la Tanzania la kufikia hadhi ya kipato cha kati, programu za USAID zimelenga kufikia ukuaji wa uchumi uliojumuishi, na endelevu, kuendeleza utawala bora wa kidemokrasia, na kuokoa maisha kwa kuboresha huduma na mifumo ya afya.

USAID pia inafanya kazi ya kuwawezesha wanawake na vijana wa Kitanzania ambao ni muhimu kwa maendeleo endelevu ya Tanzania lakini ni miongoni mwa raia waliotengwa zaidi. Mishahara ya wanawake, kwa mfano, ni wastani wa asilimia 63 chini kuliko wanavyolipwa wanaume, wakati biashara zinazomilikiwa na wanawake zinapata faida pungufu mara 2.4 zaidi. Vijana walio chini ya umri wa miaka 15 ni asilimia 45 ya idadi ya Watanzania milioni 55. Kuongeza upatikanaji wa fursa za kiuchumi na kielimu kwa vijana kutasaidia sana kuhakikisha Tanzania inaendelea kuelekea kwenye kujitegemea.

Serikali ya Marekani ndio mfadhili mkubwa wa Tanzania. USAID inashirikiana na watu wa Tanzania kufanikisha malengo ya maendeleo ya taifa kama ilivyoainishwa katika.