Language

Leo, Marekani imetoa msaada wa dola 100,000 katika juhudi za kukabiliana na maafa yaliosababishwa na mafuriko pamoja na maporomoko ya ardhi yaliyotokea mkoa wa Manyara nchini Tanzania na kusababisha vifo vya zaidi ya watanzania 70, kuharibu mashamba, na maelfu ya watu kuyahama makazi yao. Msaada huo unaotolewa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), kupitia Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, utasaidia serikali ya Tanzania katika kukabiliana na maafa yaliyotokea kaskazini mwa nchi hiyo. USAID na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC) vitaendelea kufuatilia hali hiyo na kutoa usaidizi wa ziada unapohitajika.

“Tunaomboleza pamoja na Watanzania kote nchini kutokana na mafaa haya yaliyosababisha upotevu wa maisha pamoja na makazi.” alisema Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Michael Battle. “Wafanyakazi wote kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania tunawaombea wale wote walioathiriwa na mafaa haya. Marekani inasimama na rafiki na mshirika wetu Tanzania wakati huu.” aliongeza Balozi Battle: “Serikali ya Marekani inaipongeza serikali ya Tanzania kwa uongozi wao madhubuti na hatua za haraka za kupunguza athari za mafaa na kusaidia wananchi katika mkoa wa Manyara.

Mvua kubwa imeathiri maeneo ya kaskazini mwa Tanzania tangu Oktoba wakati wa msimu wa mvua za Oktoba na Desemba 2, na kusababisha mafuriko, mito kuja na maporomoko ya ardhi. Mnamo Desemba 2, maporomoka ya ardhi yalitokea katika kijiji cha Kateshi katika Wilaya ya Hanang Magharibi mwa Manyara, na kusababisha uharibifu mkubwa ulioripotiwa. Maporomoko hayo pia yameharibu miundombinu ya umma, ikiwemo barabara, umeme, na mifumo ya mawasiliano na maji.

Kwa taarifa zaidi kuhusu taarifa hii wasiliana na ofisi ya mawasiliano Ubalozi wa Marekani kupitia: DPO@state.gov.