Language

Dar es Salaam, Tanzania - Aprili 20, Serikali ya Marekani, kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), imeendesha kikao mubashara kwa njia ya mtandao kusherehekea mafanikio ya elimu ya msingi yaliyopatikana kwa miaka mitano ya mradi wa Tusome Pamoja na miaka miwili ya mradi wa Hesabu na Elimu Jumuishi.

Hafla hiyo kwa njia ya mtandao, “Kusherehekea Miaka Mitano ya ujifunzaji wa madarasa ya awali/chini, Hesabu na Elimu Jumuishi,” ilionesha mafanikio endelevu katika usomaji, hesabu, na elimu jumuishi kwa sekta ya elimu ya awali na msingi.

“Elimu hutumika kama dira ya maendeleo mengine yote na hupunguza umaskini uliokithiri. Serikali ya Marekani, kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa, itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha ufadhili ni muhimu kwa watoto na vijana wote wa Kitanzania,” alisema Mkurugenzi Mkazi wa USAID Andrew Karas ambaye alifungua hafla hiyo kwa njia ya mtandao.

Mradi wa Tusome Pamoja unaboresha kiwango cha ufundishaji wa stadi za msingi za madarasa ya awali/chini, inaboresha njia za ufundishaji na ustadi, na inashirikisha wazazi na jamii katika kusaidia kuboresha matokeo ya elimu. Washirika wa mradi, Hesabu na Elimu Jumuishi, inaleta ufundishaji na mafunzo ya hesabu kwa walimu kujibu vizuri mahitaji ya watoto wenye ulemavu. Miradi yote miwili inashirikiana na Wizara ya Elimu Bara na Zanzibar, Taasisi ya Elimu ya Tanzania, Taasisi ya Elimu ya Zanzibar na OR-TAMISEMI na OR-TAMISEMI-Idara Maalum.

Kama mfadhili mkuu wa Tanzania, Serikali ya Marekani inatoa msaada mkubwa kwa Tanzania na inadhamini mipango anuwai katika sekta nyingi. Katika miaka mitano tu iliyopita, USAID imewekeza dola za Marekani milioni 82 katika elimu ya msingi nchini Tanzania. Hadi sasa, Mradi wa Tusome Pamoja umefikia zaidi ya watoto milioni 2.4 katika shule 3,060 na kuboresha umahiri wa kusoma, kuandika na hesabu. Kwa kuongezea, zaidi ya waalimu 20,000 wamefundishwa mbinu za kufundishia za matamshi za kusoma na kuhesabu.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwa njia ya mtandao baada ya hafla hiyo, Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Andy Karas alisema, "Tunaamini kwamba ikiwa watoto wana afya, wamelishwa vizuri, wanasomeshwa, na wanasaidiwa na walezi wao na jamii, basi watakuwa na ujuzi unaohitajika kuwa vijana wenye tija, wenye nafasi nzuri ya kufuata na kufikia matarajio yao.”

Kwa taaarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kupitia DPO@state.gov.

Image
Kusherehekea Miaka Mitano ya ujifunzaji wa madarasa ya awali/chini, Hesabu na Elimu Jumuishi
Kusherehekea Miaka Mitano ya ujifunzaji wa madarasa ya awali/chini, Hesabu na Elimu Jumuishi
USAID / Tanzania